Demokrasia ya kweli haishabihiani na Ubepari.

Yametafsiriwa na Thomas J. Kibwana.

Katika miongo miwili iliyopita, mfululizo wa migogoro umesababisha kuibuka kwa serikali za kiimla zenye kuongozwa kibabe , ikionyesha kwa dhahiri jinsi Ubepari na demokrasia havikuwa vinafungamana tokea mwanzoni.

Inazidi kuwa ngumu kupuuza ukweli kuwa hali ya demokrasia duniani kote inakumbana na anguko. Kwa upande mmoja, mataifa yenye nguvu zaidi duniani — tangu kule China hadi Saudi Arabia — yanatawaliwa na tawala za kiimla ambazo zinazidi kujilimbikizia mamlaka zaidi na zaidi. Kwa upande wa pili, heshima kwa tunu za kidemokrasia za kiliberali — kama vile haki ya kufanya maandamano na uhuru wa mahakama — inapungua katika serikali nyingi. Na mataifa mengi ambayo yaliyodhaniwa kuwa kwenye njia ya demokrasia — kama vile Hangaria na Uturuki — yamekwama toharani mwa “kisichokuwa demokrasia ya kiliberali”.

Kwa jumla, takriban asilimia 72 ya idadi ya watu duniani wanaishi chini ya aina fulani ya utawala wa kiimla, hii ni kadiri ya maoni ya wataalamui. Watafiti wa taasisi ya Freedom House wanadai kuwa takriban asilimia 38 ya idadi ya watu duniani wanaishi katika nchi ambazo zinaweza kutizamwa kama “si huru.” Mwanazuoni wa kidemokrasia, Larry Diamond, ameiita hali hii ya kurudi nyuma kwa demokrasia duniani kote “mdororo wa demokrasia.”

Mmomonyoko wa demokrasia umekuwa ni jambo gumu mno kwa waliberali kuuchambua kinadharia. Kwasababu kwao, mambo hayakupaswa kuwa kama yalivyo leo.

Kuanguka kwa ukuta wa Berlin kwao ilikuwa kama uteguzi wa kitendawili cha muda mrefu juu ya kushabihiana kwa demokrasia na ubepari. Ilitarajiwa kuwa hilo la pili (ubepari) lingetanuka na kusambaa, na kwa kufanya hivyo lingeleta haki na uhuru,vitu ambavyo watu wengi katika mataifa tajiri hawavipi uzito upasao na kuviona kuwa ni masuala tu ya kawaida. Kwa hiyo ilidhaniwa kuwa ulimwengu usio wa kimagharibi haukuwa na namna nyingine isipokuwa tu kuelekea katika muundo huo unaaongozwa na wamagharibi.

Novemba 9, 1990. Ukuta wa Berlin ukiangushwa mbele ya maelfu ya mashuhuda. Tukio hilo lilitajwa kuashiria kuanguka kwa ukomunisti duniani na mwanzo mpya wa demokrasia ya kibepari kwa ulimwengu mzima. Picha kwa hisani ya mtandao.

Wana nadharia na watunga sera wa kiliberali wamekuja na hoja kadhaa kuelezea mkanganyiko unaoonekana kuwepo baina ya kutanuka kwa ubepari na kusinyaa kwa demokrasia.

Walio katika upande wa kulia wa mrengo wa kisiasa wanajaribu kuonesha kuwa tatizo lipo kwa “maadui wa demokrasia” wa kigeni. Kwa vinara hawa wa Vita Baridi mpya, Xi Jinping na Vladimir Putin — ingawa cha kushangaza hawawataji Mohammed bin Salman au Viktor Orbán — kwamba wanapaswa kulaumiwa kwa kuhadaa watu wapenda demokrasia Magharibi kupitia propaganda ya kiimla.

Wale wa mrengo wa kati hudai kwamba tatizo halisi ni “wenye msimamo mkali pande zote,” hujenga hoja kwamba wanasiasa wa Ujamaa wa kidemokrasia kama Bernie Sanders na Jeremy Corbyn, ambao hawajawahi hata kukaribia kushika madaraka ya nchi, wanapaswa kubeba lawama sawasawa na viongozi wa zamani katika upande wa mrengo wa kulia kama Boris Johnson na Donald Trump.

Kila tathmini ya tatizo [kati ya hizo tajwa], kimsingi inatizama tatizo kwa ngazi ya mtu binafsi. Wengi wa waliberali wanadhani kwamba changamoto kubwa kwa demokrasia leo ni “watu wachache wabaya” wanaoharibu mfumo ambao kwa ujumla unafanya kazi vizuri.

Hoja hizi ni za kipuuzi kabisa. Ungwaaji mkono wa demokrasia haupungui kwa sababu wapiga kura wanahadaiwa na propaganda ya maadui kwenye katika mtandao TikTok. Ungawaji mkono wa demokrasia unapungua kwa sababu demokrasia haifanyi kazi kama tulivyokuwa tukielezwa ingfanya.

Awali, mchanganyiko wa ubepari na demokrasia ulitarajiwa kuwa ungeleta utajiri na maendeleo kwa mataifa yote yaliyolikumbatia hilo. Katika muda mfupi baada ya kuanguka kwa Ukuta wa Berlin, wakati utandawazi ulipokuwa kwa kasi, hii ilionekana kuwa ni hadithi inayopaswa kuaminika.

Mgogoro wa kifedha ukautamatisha “udanganyifu huu wa jumla” katika Ulimwengu wa Kaskazini [mataifa yaloendelea]. Wanachama wa kizazi kilichopevuka wakati wa mgogoro wa mwaka wa kiuchumi wa 2008 walilazimika kukubaliana na ukweli kwamba hakukuwa na uwezekano kwa wao kuwa na hali bora kuliko ya wazazi wao.

Lakini hata kabla ya mgogoro wa kifedha, mgogoro wa Asia mwishoni mwa miaka ya 1990 ulionyesha wengi katika ulimwengu unaoendelea kwamba kufungua masoko yao kwa mtaji wa kimataifa kunaweza kuwa mwanzo wa janga. Kwa hivyo mchanganyiko fulani wa udikteta na udhibiti wa masoko ulionekana kama jawabu mujarabu la kiasili.

Pili, hatua zilizoletwa na demokrasia na ubepari yzilipaswa kuzaa demokrasia zaidi. Mipaka na usawa ingekomesha ufisadi. Watu wenye elimu wangechagua viongozi “sahihi.” Na badala ya kampeni kulingana na ideolojia zilizopitwa na wakati, viongozi hao wangekuwa wanashindana kwa kura kwa kuvutia “mpiga kura wa wastani,” wakileta usawazishaji katika jamii zilizokuwa zimegawanyika awali.

Badala yake, ufisadi unaongezeka, ideolojia zimeibuka tena, na watu wanaendelea kuchagua viongozi “wabaya.” Labda uumbaji wa jamii zenye matabaka makubwa kiasi ambacho, tabaka tawala haliwezi kujali kabisa wasiwasi wa wapiga kura wa kawaida, muarobaini kwaajili ya demokrasia.

Baadhi ya wachambuzi makini zaidi hukubali kwamba, namna hii ya kuchambua na kubainisha mambo kirahisi rahisi kunaleta hatari ya kutolizingatia jambo katika utimilifu wake. Katika mfululizo mpya wa podcast wa Financial Times, Martin Wolf anaonekana kuwa na wasiwasi halisi kuhusu mustakabali wa demokrasia — na anakubali sehemu ndogo ya lawama kwake yeye mwenyewe na wenzake.

Kwa mujibu wa Wolf, tatizo linaonekana kuwa ni kwamba waliberali, kwa hamu yao yote ya “Mwisho wa Historia”[Mwisho wa historia ni dhana ilioibuliwa na mwanazuoni wa kimarekani Francis Fukuyama, baada ya anguko la ukomunisti huko Ulaya ya mashariki], walipanua masoko huru kwa kasi na mbali sana. Tiba-mshtuko ya miaka ya 1990 haikupatana na hatua za kupunguza mivutano ya kijamii na kiuchumi iliyoambatana na janga lenyewe.

Hoja hii hukumbusha wa kile kilichotolewa na mwanafikra wa mrengio wa kimaendeleo Karl Polanyi, ambaye aliamini kwamba masoko huru ya kibepari yalipanuka kwa kasi sana kiasi kwamba jamii nyingi kushinda kuendanda na kasi ya msambao huo. Wale ambao maisha yao na tunu zao zilitishiwa na kujitokeza kwa dunia hii mpya yenye changamoto wangekabiliana na hali hiyo ya uvamizi wa “jamii ya soko” — mara nyingi kwa kuunga mkono viongozi wababe wa kiimla wenye kufanya hivyo.

Read More: True Democracy Is Incompatible With Capitalism

Waliberali wa kimaendeleo kama Wolf wanaamini kwamba suluhisho la tatizo litapatikana katika aina fulani ya ubepari unaosimamiwa na kuratibiwa. Mara nyingi, wachambuzi hawa ni wanafikra ya “Keynesia” ambao wanapigia debe kurudi kwa kauli ya maafikiano ya kidemokrasia ya kijamii baada ya vita.

Lakini aina hii ya ukumbusho si bora zaidi kuliko ule unaodhihirishwa na wafuasi wa Trump wanaotamani kurudi kwenye ulimwengu kabla ya kusambaa kwa “ideolojia ya jinsia.” Hatimaye, ipo, sababu ya ni kwa nini makubaliano ya Keynesia yalimeguka vipande.

Pindi tu ukuaji wa uchumi ulipozorota, ugomvi uliokuwa umefichika baina ya wafanyakazi na wamiliki wa biashara ambao ulilipuka ghafla kuja hadharani kama jambo la kisiasa. Bila faida-ziada kubwa zilizochotwa kutoka kwa ulimwengu ili kuuzima mzozo, kulikuwa na chaguo moja tu kwa tabaka tawala: vita kamili dhidi ya wafanyakazi.

Kwa sababu hii, licha ya ukweli kwamba ni dhahiri kabisa kwamba nchi za demokrasia ya kibepari zinahitaji hatua fulani ili kupunguza pengo la hali ya ukosefu wa usawa huku zikikabiliana na suala la janga la tabia nchi, fikra ya umaendeleo ya kibepari kwa ajili ya siku zijazo haiwezi kutekelezeka.

Kuna hitimisho moja tu linalosalia kufikiwa — kwamba ubepari na demokrasia havijawahi kwamwe kuwa vinavyoendana tangu awali.

Leave a comment

SAUTI YA UJAMAA

Welcome to the Socialist Voice

Discover WordPress

A daily selection of the best content published on WordPress, collected for you by humans who love to read.

The Daily Post

The Art and Craft of Blogging

WordPress.com News

The latest news on WordPress.com and the WordPress community.