Category DARASA LA ITIKADI

AZIMIO LA MANZESE (THE MANZESE RESOLUTION)

AZIMIO LA MANZESE JUU YA KUBOMOA MIFUMO YA KINYONYAJI YA UKOPESHAJI FEDHA NA KUJENGA MIFUMO MBADALA INAYOENDESHWA NA KUMILIKIWA NA WANYONGE Sisi wanawake, wengi wetu tukiwa ni wanyonge tunaojishughulisha na biashara ndogo ndogo katika jiji la Dar es Salaam, tumekutana leo tarehe 9 Marchi 2019 katika eneo la Manzese kwa ajili ya kuadhimisha Siku ya […]

TAASISI YA ROSA LUXEMBURG KUZINDUA “TUZUNGUMZE FILAMU”

Taasisi ya Rosa Luxemburg ni asasi ya kimataifa inayotoa jukwaa kwa ajili ya tafiti, elimu ya kiraia na mijadala ya mrengo wa kushoto. Moja ya miradi ya Taasisi hii hapa nchini Tanzania ni Tuzungumze Filamu, ambao unahusisha utumiaji wa filamu kama zana ya kujifunza na kuendesha mijadala juu ya sera za maendeleo. Mradi huu unalenga kutoa […]

DARASA LA ITIKADI KUMWENZI BOB MARLEY

Katika darasa la Jumamosi tarehe 10 Februari 2018, tutakuwa na mjadala kuhusu “Nafasi ya Sanaa katika mapambano ya wavujajasho”. Kama tulivyokubaliana darasani wiki iliyopita kwamba marejeo kwa ajili ya mjadala huu ni pamoja na dhima na maudhui ya nyimbo za hayati Bob Marley ambaye wiki hili ilikuwa ni kumbukizi ya kuzaliwa kwake. Pia, tutaangazia baadhi […]

KISA CHA MABINTI WAPAMBANAJI KATIKA RIWAYA YA “THE BANANA GIRLS” (1)

Na Joel Ntile “Je wajua kwamba hizi ndizi (banana) unazokula zimepindua serikali halali nyingi duniani na kuyafukarisha mataifa mengi? Ndio, ni ndizi hizi hizi, moja ya tunda linalotumiwa zaidi ulimwenguni. Historia yake, uzalishaji wake na uuzaji wake kwa pamoja huashiria namna ya siasa za ndani ya taifa na za kimataifa zilivyo. Kuelewa hilo kiundani haikuhitaji […]

NASH MC: UBEPARI NDIO CHANZO CHA MATATIZO YETU

Jukwaa la Wajamaa tumekuwa tukijenga mshikamano na vuguvugu la muziki wa kimapinduzi kwa lengo la kuunganisha nguvu katika mapambano dhidi ya ubepari. Vuguvugu hilo hapa nchini linahusisha ‘wasanii marufuku’ ambao wamekataa katakata kulisujudia kundi lililohodhi tasnia ya muziki, ambalo sio tu hunyonya nguvu-kazi ya wasanii, lakini pia huwalazimisha wasanii kuimba nyimbo zisizo na maudhui ya […]

2018: MWAKA WA KUUHUJUMU UBEPARI

Hatujifichi: kwetu sisi JULAWATA tutauanza mwaka 2018 kwa kuongeza jitihada zaidi za kuuhujumu ubepari hapa nchini, ili uanguke – kama ambavyo wao mabepari waliuhujumu ujamaa. Tutahakikisha kuwa mashirika ya umma yaliyobinafsishwa yanarudi mikononi mwa serikali. Na mashirika ya umma yaliyo mikononi mwa serikali hayawafaidishi mabepari au warasimu serikalini – bali yanawafaidisha wanyonge nchi hii. Tutashirikiana […]

KUFURAHI NA UJAMAA: HAKI YA KUFURAHI NA VITA DHIDI YA UBEPARI

Na Melki Kabalu Lulandala Ilikuwa siku ya Jumamosi ya tarehe 23/9/2017, siku ambayo Jukwaa la Wajamaa Tanzania liliamua kukutana katika fukwe maarufu za “Coco” (Coco Beach) jijini Dar es salaam. Furaha na mazungumzo vilitawala, utani na vicheko navyo vilisikika kwa wingi, picha za “kujipiga” (selfie) zilipigwa kwa wingi kabisa, huku nyimbo mbalimbali za kuamsha ari […]

WAJUKUU WA A. M. BABU NA TAFAKARI YA UJAMAA KATIKA AFRIKA!

Ilikuwa juma jingine tena, Jumamosi ya Tarehe 2 Septemba, ambapo Jukwaa la Wajamaa Tanzania lilikutana katika Darasa la Itikadi kuzipa tafakari fikra za Mzee wetu na Kamaradi Abdulrahman Babu juu ya Ujamaa. Na katika hatua hii tuliangazia andiko la Kamaradi Babu “Ujamaa wa ki-Afrika au Afrika ya Kijamaa?” (African Socialism or a Socialist Africa?). Mazungumzo na […]

MARCUS GARVEY NA UKOMBOZI WA AFRIKA

Na Sabatho Nyamsenda Kwa wengi, hasa wale waliozaliwa katika miongo mitatu iliyopita, jina la Marcus Garvey litakuwa geni masikioni mwao. Wachache wanaweza kuwa wamelisoma katika vitabu vya historia, lakini kwa juu juu tu. Na hii ndio sababu kuu iliyowafanya Taasisi ya Marastafari Tanzania (Rastafari United Front – RUF) kuandaa kumbukizi kwa ajili ya kutabaruku mchango […]

UDUGU KUSEMEZANA

Jua lilikuwa kwenye MGOMO. Wingu lilitanda haswa; na licha ya kuwa bado mchana, mandhari ya kiza kiza siku ya Jumamosi, 29/04/2017, yalisema vinginevyo. Lakini si mvua na si jua vingeweza kutukwamisha katika azma yetu ya kufika UBUNGO STENDI YA MKOA na KUSEMEZANA na NDUGU zetu MADEREVA.   “Vijidimbwi na Midimbwi” (Madimbwi) tuliruka na wakati mwengine […]

MAKAMPUNI YA KINYONYAJI, UDHAIFU WA DHANA YA “UTOAJI MISAADA”, NA UPOTOSHAJI WA WASEMAJI WAHAMASISHAJI (INSPIRATIONAL SPEAKERS)

Propaganda ni nyingi sana katika kuhalalisha unyonyaji na kuficha mahusiano yaliyopo baina ya umasikini na utajiri

SAUTI YA UJAMAA

Welcome to the Socialist Voice

Discover WordPress

A daily selection of the best content published on WordPress, collected for you by humans who love to read.

The Daily Post

The Art and Craft of Blogging

WordPress.com News

The latest news on WordPress.com and the WordPress community.