Tunapenda kuwafahamisha wasomaji wetu ndani na nje ya Afrika kuwa blogu ya SAUTI YA UJAMAA inamilikiwa na kuratibiwa na Bwana NJUKI GITHETHWA ambae ni raia wa Kenya. Blogu hii itaendelea kuchapa makala zinazohusu mapambano ya wavujajasho ndani na nje ya Afrika, huku msisitizo mkubwa ukiwa katika nchi za Afrika Mashariki. Tunawaalika wasomaji wetu watume makala […]

Kwa KARNE na KARNE, Bara letu la AFRIKA limedhulumiwa haki na stahiki yake ya kujipatia na kuyafikia MAENDELEO YA KWELI – kwa watu wake WOTE. Ni dhahiri kuwa dhana ya MAENDELEO YA KWELI ni tofauti na AJENDA YA MAENDELEO kama inavyohubiriwa (au kudaiwa “kupiganiwa”) na nchi za Magharibi. Wakati JAMII zetu zikiendelea kulishwa PROPAGANDA na kuaminishwa vingine juu hali yetu ya […]

BARUA YA “SIRI” KWA RAIS NDG. SAMIA SULUHU HASSAN Na, Muhemsi C. Mwakihwelo Utangulizi Ndg. Rais, ninakusalimu na kukutakia heri. Ninakutakia heri kwa kuwa ninaamini ya kwamba heri kwako inapaswa kuakisi heri ya walio wengi katika taifa letu. Waraka huu ni wa siri kwako na sikupenda kuufanya kuwa wa wazi kwa sababu nitakaoziainisha hapo chini, […]

IN REVOLUTIONARY MEMORY OF AMILCAR CABRAL. 50 YEARS AFTER HIS DEATH ON JANUARY 20, 1973.

Tarehe 30 Juni, 1960, Waziri Mkuu wa kwanza wa Kongo, Patrice Lumumba, alisimama kuhutubia si tu wanasiasa waliokusanyika bungeni na wabelgiji wachache wa tabaka la juu waliokuwa katika hali ya kimuhemuhe,bali pia watu wake waliokuwa wamekombolewa upya.  Na; Patrice Emery Lumumba Msanifu Mchoro; Anastasya Eliseeva Imetafsiriwa kwa lugha ya kiswahili na; Muhemsi C. Mwakihwelo. Mabibi […]

Na Muhemsi Mwakihwelo Kimya mshindo mdogo, hali tete mtaani Ukwasi watupa chogo, sononi tele moyoni Mafanikio kwa wigo, bado tumo mkwamoni Hakujafana kayani, watwelemea mzigo. Adha hakuna fahari, miyaka nenda na rudi Raiya na askari, ukata hatufaidi Kivipi tujisitiri, uzito usituzidi? Tumechoshwa na ahadi, zisoshindwa tusitiri. Changamoto zi lukuki, nyanja zote maishani Mfumuko hushikiki, gharama […]

Na; Muhemsi C. Mwakihwelo Bwana weye nisikiye, shauri langu nitowe Tena usinipuziye, nia we rahimu uwe Mpangaji niridhiye, ili kesho sizomewe Haki usinondoleye, nakuwasa nielewe. Bwana weye uelewe, upangaji si uduni Yanini uwe kiwewe, kwanini unilaani Mpangaji seshimiwe, wewe wafaidi nini Haki ninasitahiki. nakuwasa nielewe. Bwana weye una nini, wanitusi mi fukara Wasahau kwa yakini, ninakulipa ujira […]

By; Muhemsi C. Mwakihwelo The dates from the 12th to the 16th of August 2012 witnessed a standstill moment in South Africa which ought to reverberate for many years to come. Those were indeed the days of darkness as they were filled with disturbing and horrible scenes and imagery of bloodshed. The modern-day South African […]

Wakulima Wadogo Jibuni! Na Muhemsi Mwakihwelo. Umetimu mwezi mmoja sasa tangu egemeo la utulivu wa kisiasa ndani ya chama cha mapinduzi (CCM) kupata mushkeli ambao iliwawia vigumu mno hata waandamizi wa chama hicho kuficha kuwa wametingishwa na hali hiyo. Ukisoma kitabu cha muinjili Luka mtakatifu sura ya 23 hasa mstari wa 18 unapata kujua namna […]

Nianze kwa simulizi ya mazungumzo baina yangu na rafiki yangu mmoja na mshirika wa kifikra katika  umajumui wa Afrika ambaye kwasababu kadhaa si miongoni mwa watu wangu wa karibu kwa sasa. Kwa njia ya simu asubuhi moja majira ya kiangazi 2015 nikielekea shamba yeye akiniarifu kuwa alikuwa mkoa mmoja huko kanda ya ziwa, nalizungumza naye […]

Sisi wanawake wavujajasho wa mjini na vijijini tunaojumuisha wafanyabiashara ndogondogo na wakulima wadogo, tumejumuika kimshikamano kusherehekea siku ya wanawake wavujajasho duniani leo tarehe 8/3/2022 katika ukumbi wa Amy Garvey  Manzese. Tukiwa  kama wanawake  tunaokumbana na madhila mbalimbali chini ya mifumo yote kandamizi, tunatambua kuwa maslahi yetu ni tofauti na maslahi  ya wanawake wa tabaka la juu. […]

“Israel should once again be an observer state of the African Union … I fervently believe that it’s in your interest too, in the interest of Africa. And I hope all of you will support that goal,” Benjamin Netanyahu told West African leaders at the 51st ECOWAS Summit of Heads of State in Liberia’s capital Monrovia ,2017. […]

Wavuja jasho lazima waelewe hayo ili wasihadaiwe na siasa za madaraka zenye lengo tu la kushika dola hilihili lenye sifa za kikoloni.Kulipa jina la Tanganyika ama Tanzania hakuliondolei sifa hizo,hivyo suluhu kwao si uwepo serikali ya Tanganyika. Kwa zama nyingi kumekuwako na hulka ya watu kutaka/kutamani mapungufu,kushindwa ama uzembe wao uwe umetokana na watu ama […]

Na, Muhemsi Mwakihwelo Kwa kuwa, hakuna kisichobadilika isipokuwa mabadiliko yenyewe basi ni haki kwetu kujumuisha kuwa hata wasingekuja hapa nchini kwetu wamishonari, wapelelezi na wafanyabiashara kutoka mataifa ya Ulaya(hasa Ulaya magharibi) nchi yetu isingesalia vilevile kama ilivyokuwa katikati ya karne ya 19. Ni ngumu kutoa taswira sahihi ya nini kingejiri na ni hatari kugeukia katika […]

SAUTI YA UJAMAA

Welcome to the Socialist Voice

Discover WordPress

A daily selection of the best content published on WordPress, collected for you by humans who love to read.

The Daily Post

The Art and Craft of Blogging

WordPress.com News

The latest news on WordPress.com and the WordPress community.