SHAIRI: AZIMIO@57

NA ISSA BIN MARIAM

nilizaliwa sitini na saba

nimefikisha hamsini na saba

nilizaliwa Arusha

jiji kasoro bahari

nikazikwa Zanzibar

kisiwa kinachoelea baharini

naitwa majina mengi

natambulika kwa sifa moja

waasisi huniita Azimio la Arusha

makada Azimio la TANU

wajipendekezao hunipamba Azimio la Nyerere

wajinga hunikejeli Azimio la Mussa

naitwa majina mengi

natambulika kwa sifa moja

mwiba kwa wanyonyaji

maua kwa wanyonge

kero kwa fanyiwakazi

matumaini kwa wafanyakazi

nilizaliwa hospitali ya Mapambano

nikakulia kiwandani MountCaramel

mjukuu wa MamaNtilie

mpendwa wa hohehahe

uhai wangu uliwasumbua

ukuaji wangu uliwatesa

siku na mchana

bila mapumziko, bila raha

gizani na vichakani

wakapanga wakapangua

mipango yao michafu ya kuniua

hatimaye wakanizamisha baharini Hindi

endeleeni kuipa barabara zenu

5-star zenu, viwanda vyenu, miradi yenu

jina la mhenga wangu

eti mnamuenzi kwa kumjengea sanamu

wakati mnamdhalilisha kwa kubomoa usanifu

wa Taifa lililojengwa kwa jasho na damu. 

mzimu wangu utaendelea kuwatesa

fikra zangu zitaendelea kuwasumbua

nitafufuka kwa majina ya kidigitali

nitawafuata hekulini

nitahamahama mitandaoni

nitaimba hotelini

05/02/2024

One comment

  1. Anonymous · · Reply

    Swadakta

    Asante Profesa Issa bin Mariam

    Like

Leave a comment

SAUTI YA UJAMAA

Welcome to the Socialist Voice

Discover WordPress

A daily selection of the best content published on WordPress, collected for you by humans who love to read.

The Daily Post

The Art and Craft of Blogging

WordPress.com News

The latest news on WordPress.com and the WordPress community.