JOTO LA KITABAKA NA MWELEKEO WA KIMAPINDUZI (2)

Na Gikaro B. Makera

Wakoloni na washirika wao ambao ni Waafrika makomprodari walijihusisha na mkakati uliongozwa na kile Mwanafikra wa nadharia ya mapambano ya wavujajasho Walter Rodney alichokiita “Fikra za kinjama za kihistoria”(Conspiracy theories of history) na hatimaye walikabidhiana uhuru lakini kwa masharti ya kuendeleza mahusiano ya kikoloni (ya-kinyonyaji) katika nchi zao, na hili ilisababisha kuendelea kuwapo mgongano huo wa kimaisha, mfano hapa kwetu Tanzania inaelezwa kuwa kulikuwa na walioitwa wabenzi  na baba kabwela. Uhalisia tunaouona hapa unaonesha ni kosa kusema kuwa Afrika hakukuwa na matabaka; Tunashukuru historia na uzoefu wa maisha yenyewe imelitanabaisha hilo. Pia tunawashukuru Nkrumah na Nyerere kusahihisha hilo kwa kudhihirisha kwamba kulikwepo na matabaka katika jamii zetu. Mwalimu Nyerere (1970) alikiri wakati akihutubia shirika la Katoliki la Mary-Knoll huko New York Marekani anachambua hivi,

“Tatizo la Dunia ya leo (Kibepari) si umasikini maana tunao ujuzi na amali zinazotuwezesha kufuta umasikini. Tatizo lenyewe hasa ni mgawanyiko wa binadamu katika tabaka mbili, tabaka ya matajiri na tabaka ya masikini. Jambo hilo ndilo linaloleta vita, chuki kati ya watu”(J.K Nyerere: Binadamu na maendeleo).

Mwalimu Nyerere hakuishia tu kutambua mpasuko huo ila pia alitoa suluhu ya kisayansi ya kumaliza kabisa mpasuko huo  katika hotuba yake akiwa Mbeya mwaka 1995 siku ya wafanyakazi (wavujajasho) Duniani (Mei Mosi) alilisihi sana tabaka la wavujajasho kuungana na kushikamana na hatimaye kuubomoa mfumo huo unaochechea uwepo wa matajiri wachache na masikini(wavujajasho) wengi na alitumia kauli mbiu ya wavujajasho ya muda wote  kuonyesha msisitizo juu ya hilo “Enyi wavujajasho wote unganeni. Hamna cha kupoteza ispokuwa minyororo ya utumwa mliofungwa”.  Kwa upande mwingine Nkrumah naye alionyesha mkakati wa kisayansi unaoweza kutumiwa na wavujajasho baada ya kuungana na kuangusha mfumo huo,katika chapisho lake la (Hand book revolutionary warfare,1968).

Adui ni nani?  

Sehemu ya  makala haya ni kujaribu kufuta mawazo ambayo yametawala zaidi kwa muda wa nusu karne hapa Tanzania na Afrika kwamba kumekwepo madui wa tatu katika jamii zetu hizi za kibwenyenye ambao hao madui  watatu  hutajwa kuwa ni Umaskini,ujinga na maradhi.

Kudhani hivi vitatu ndio chanzo cha matatizo katika jamii zetu ni kupoteza muda tu. Ndiyo maana kwa muda mrefu hasa baada ya kutupwa kwa Azimio la wanyonge (Azimio La Arusha) kumekwepo na mikakati mbali mbali ya kupambana na vitu hivi tatu bila mafanikio. Kwa mfano mkakati wa kurekebisha uchumi uliokuwa na sera za soko huria na ubinafsishaji ambao uliletwa  katikati mwa miaka ya 1980 kama suluhisho la udumavu huo lakini badala yake huo mpango umezidisha ulikimbizaji  wa mitaji (utajiri) kwenye upande mmoja mdogo, na kwa  wakati huo huo mmoja, mpango huo uchumi umezidisha ulimbikizaji wa mateso, maradhi, ujinga, umaskini, utumwa, , maumivu makali (agony), ukatili (brutality) upunguani au uzezeta wa akili (Mental degradation) katika upande mwingine mkubwa ambao ndio ule wa wavujajasho.

Sasa kutokana na uzoefu wa kihistoria tunapaswa kukifiria kabisa kwamba chanzo  na adui wa wavujajasho si Umasikini,maradhi au ujinga bali hivi ni matokeo tu ya mahusiano ya kikoloni ambayo yamejikita katika hulka ya uhodhi binafsi na unyonyaji wa kazi/jasho la wengi na kupelekea kubakia duni na kuchochea matabaka, kati ya walalahoi na wenye uhodhi wa mali .

Hiki ndicho hata Mwalimu Nyerere alikisitiza sana katika kipindi cha uhai wake hasa baada ya kutangazwa Dira ya maendeleo ya wavujajasho (Azimio La Arusha). si Mwalimu tu alisisitiza bali hata wavujajasho wenyewe toka ukoloni mpaka sasa kwenye ukoloni mambo-leo wameendelea kupambana na kuielezea hali hiyo. Mfano mzuri ni Mateo Izodory kwa niaba ya wavujajasho wenzake ililielezea hili katika Makala yake iliyochapishwa katika safu ya SAUTI YA MSHIKAMANO ya  Gazeti la Raia Mwema la January 7-8,2019, anasisitiza kwamba adui mkubwa wa maisha ya wavujajasho na jamii kiujumla ni kukithiri kwa mahusiano yaliyojikita katika unyonyaji ambapo wao kwa mfano Boda boda hufanya kazi ngumu na kubwa na kuwaingizia mabossi wao faida kubwa  ila huishia kupata ujira kiduchu ambao hata kukidhi mahitaji yao ya kila wakati inashindikana na hivo kuchochea umasikini, Maradhi na ujinga  mkubwa kwa maana hushindwa kumudu gharama za matibabu na kusomesha watoto wao…. (Itaendelea)

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

SAUTI YA UJAMAA

Welcome to the Socialist Voice

Discover WordPress

A daily selection of the best content published on WordPress, collected for you by humans who love to read.

The Daily Post

The Art and Craft of Blogging

WordPress.com News

The latest news on WordPress.com and the WordPress community.

%d bloggers like this: