Kwa KARNE na KARNE, Bara letu la AFRIKA limedhulumiwa haki na stahiki yake ya kujipatia na kuyafikia MAENDELEO YA KWELI – kwa watu wake WOTE. Ni dhahiri kuwa dhana ya MAENDELEO YA KWELI ni tofauti na AJENDA YA MAENDELEO kama inavyohubiriwa (au kudaiwa “kupiganiwa”) na nchi za Magharibi.
Wakati JAMII zetu zikiendelea kulishwa PROPAGANDA na kuaminishwa vingine juu hali yetu ya “UMASIKINI au UDUMAVU WA MAENDELEO” sisi WAJAMAA TANZANIA tunalenga kuzizima PROPOGANDA zote, kwa hoja na mifano dhahiri, zinazolenga kuhadaa na kuuyumbisha ukweli kuwa matatizo yetu yote yanatokana na MFUMO huu DHALIMU na TAPELI wa KIBEPARI.
Kwa mantiki hii, Wajamaa Tanzania tunaukataa UBEPARI na nduguze – Utandawazi, Uliberali na wengine wengi – ambao hawana lengo la kufanikisha UKOMBOZI WA KWELI kwa Wananchi na Wanajamii WOTE.
Kupitia JUKWAA hili na shughuli nyengine nyingi katika jamii zetu, tunalenga kuibua hisia na kuamsha ari ya uelewa juu ya ADUI WA KWELI ambae ni MFUMO wa ambao umesimikwa kwa KARNE NA KARNE.
Karibu Tusemezane UJAMAA. Karibu katika MAPINDUZI!
UJAMAA JANA! UJAMAA SASA! UJAMAA DAIMA!